Norovirus

Norovirus
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuDawa ya dharura, ugonjwa wa watoto
DaliliKuhara, kutapika, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeSaa 12 hadi 48 baada ya kuambukizwa[1]
MudaSiku 1 to 3[1]
VisababishiNorovirus[2]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili[2]
KingaKunawa mikono, kuuwa virusi kwenye maeneo yaliyoambukizwa[3]
MatibabuHuduma ya kusaidia (kunywa maji ya kutosha au viowevu vya kupitia kwa mishipa)[4]
Idadi ya utokeaji wakeMatukio milioni 685 kwa mwaka[5]
Vifo200,000 kwa mwaka[5][6]

Norovirus (wakati mwingine hujulikana kama mdudu wa kutapika wakati wa baridi) ni sababu ya kawaida ya kuvimba kwa tumbo na matumbo (gastroenteritis).[7][5]

Maambukizi yake yanaonyeshwa na kuhara ambako hakuna damu, kutapika na maumivu ya tumbo.[1][2] Homa au maumivu ya kichwa yanaweza pia kutokea.[1] Dalili zake za kawaida hutokea masaa 12 hadi 48 baada ya kuambukizwa, na ahueni kwa kawaida hutokea ndani ya siku 1 hadi 3.[1] Matatizo hayatokei kwa kawaida, lakini yanaweza kujumuisha upungufu wa maji mwilini, hasa kwa vijana, wazee, na wale walio na matatizo mengine ya afya.[1]

Kwa kawaida virusi hivi huenezwa kwa njia ya vijidudu (virusi, bakteria, au vimelea) kutoka kwa kinyesi cha mtu aliyeambukizwa kuingia mwilini kupitia mdomo.[2] Hili linaweza kuwa kupitia chakula au maji yaliyochafuliwa au kuwasiliana na mtu hadi mtu.[2] Ugonjwa huu unaweza pia kuenea kupitia nyuso zilizochafuliwa au kupitia hewa kutoka kwa matapishi ya mtu aliyeambukizwa.[2] Sababu za hatari ni pamoja na utayarishaji wa chakula usio safi na kushiriki maeneo ya karibu.[2] Utambuzi wake kwa ujumla hutegemea dalili.[2] Upimaji wa uthibitisho wake kwa kawaida haupatikani, lakini unaweza kufanywa wakati wa milipuko na mashirika ya afya ya umma.[2]

Kinga dhidi yake inahusisha kunawa mikono kwa usahihi na kuondoa maambukizo kwenye nyuso zilizochafuliwa.[3] Vitakaso vya mikono vinavyotokana na pombe vinaweza kutumika kwa kuongeza, lakini havina ufanisi kuliko kunawa mikono.[3] Hakuna chanjo au matibabu maalumu ya norovirus.[3][4] Usimamizi wake bora unahusisha utunzaji wa usaidizi kama vile kunywa viowevu vya kutosha au viowevu vya kupitia ndani ya mishipa.[4] Viowevu vya urejeshaji maji mwilini ndivyo vinywaji vinavyopendekezwa kunywewa, ingawa vinywaji vingine visivyo na kafeini au pombe vinaweza kusaidia.[4]

Norovirus husababisha takriban matukio milioni 685 vya magonjwa na vifo 200,000 ulimwenguni kote kwa mwaka.[5][6] Ni kawaida katika ulimwengu ulioendelea na unaoendelea.[2][8] Wale walio chini ya umri wa miaka mitano huathirika zaidi, na katika kundi hili husababisha vifo 50,000 hivi katika ulimwengu unaoendelea.[5] Maambukizi ya Norovirus hutokea mara nyingi zaidi wakati wa miezi ya baridi.[5] Mara nyingi hutokea katika milipuko, hasa kati ya wale wanaoishi katika maeneo ya karibu.[2] Nchini Marekani, ugonjwa huu ndio sababu ya karibu nusu ya magonjwa yote yanayotokana na chakula.[2] Virusi hivi vimepewa jina la jiji la Norwalk, Ohio, ambapo mlipuko wake ulitokea mwaka wa 1968.[9]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Norovirus Symptoms". CDC (kwa American English). 24 Juni 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 Brunette, Gary W. (2017). CDC Yellow Book 2018: Health Information for International Travel. Oxford University Press. uk. 269. ISBN 9780190628611. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-29. Iliwekwa mnamo 2017-12-29.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Preventing Norovirus Infection". CDC (kwa American English). 5 Mei 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 "Norovirus - Treatment". CDC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 "Norovirus Worldwide". CDC (kwa American English). 15 Desemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "Global Burden of Norovirus and Prospects for Vaccine Development" (PDF). CDC. Agosti 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 29 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Norovirus (vomiting bug)". nhs.uk. 2017-10-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-12. Iliwekwa mnamo 8 Juni 2018.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Nguyen GT, Phan K, Teng I, Pu J, Watanabe T (Oktoba 2017). "A systematic review and meta-analysis of the prevalence of norovirus in cases of gastroenteritis in developing countries". Medicine. 96 (40): e8139. doi:10.1097/MD.0000000000008139. PMC 5738000. PMID 28984764.{cite journal}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Vesikari, Timo (2021). "25. Norovirus vaccines in pipeline development". Katika Vesikari, Timo; Damme, Pierre Van (whr.). Pediatric Vaccines and Vaccinations: A European Textbook (kwa Kiingereza) (tol. la Second). Switzerland: Springer. ku. 289–292. ISBN 978-3-030-77172-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-10-20. Iliwekwa mnamo 2023-10-05.