Papa Gregori XII

Papa Gregori XII (kwa Kilatini: Gregorius XII; kwa Kiitalia: Gregorio XII; 1326/1345 - 18 Oktoba 1417) alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Novemba/19 Desemba 1406 hadi tarehe 4 Julai 1415 chake[1]. Alitokea Venezia, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Angelo Corraro, Corario, au Correr.
Alimfuata Papa Inosenti VII. Alikubali kujiuzulu ili kumaliza Farakano la Kanisa la Magharibi (Western Schism) akafuatwa na Papa Martino V.
Baada ya kupinga madai ya wapinzani wake, Papa Benedikto XIII wa Avignon na mapapa wa Pisa, Alexander V na Yohane XXIII, akitamani kuleta umoja ndani ya Kanisa, kwa hiari yake alijiuzulu mnamo 1415 ili kumaliza mpasuko huo. [3]
Tazama pia
Tanbihi
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Riccoboni, Bartolomea (2000). Life and Death in a Venetian Convent: the chronicle and necrology of Corpus Domini, 1395–1436. Chicago & London: The University of Chicago Press. ku. 60–63. ISBN 0-226-71789-5.
Viungo vya nje
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Gregori XII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |